UGANDA: Wanafunzi wa chuo kikuu waandamana na kuvamia kituo cha polisi – Video

UGANDA: Wanafunzi wa chuo kikuu waandamana na kuvamia kituo cha polisi - Video

Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wamevamia kituo cha polisi, kudai kuachiliwa huru kwa wenzao 15 waliokamatwa walipokuwa wakiandamana dhidi ya kuongezeka kwa karo ya masomo iliyoidhinishwa mwaka jana.

Wanafunzi 15 walikamatwa siku ya Jumatatu walipokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea katika ofisi ya rais Yoweri Museveni kumuomba aingilie kati mzozo huo , limeripoti gazeti la Daily Monitor.

Picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Twitter zinaonyesha wanafunzi hao wakikamatwa nje ya lango la Chuo kikuu na wanajeshi pamoja na polisi.

Walichukuliwa katika kituo cha polisi cha Wandegeya huku wakisubiri upelelezi ufanyike, limesema gazeti hilo.Wanafunzi wenzao walivamia kituo cha polisi Jumanne kudai waachiliwe huru.

Ongezeko la 15% liliidhinishwa na baraza la Vyuo viku nchini Uganda. Wanafunzi wanatakiwa kuanza kulipa ada yenye ongezeko hilo kwa miaka mitano ijayo baadaye kila mwanafunzi atatakiwa kulipa 75% zaidi.

Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi na kijamii nchini Uganda Akol Amazima anasema ”Wasimamizi wa vyuo vikuu wanapaswa kutafuta njia za kuhakikisha kwamba wanapata pesa za kuendesha shule ili kupunguza maandamano kama hayo”

Unaweza pia kusikiliza:

Mwanafunzi aunda mabomu ya machozi Uganda
Chanzo BBCBy Ally Juma.

Related Articles

Back to top button