Afya

Uganda yafunga shule siku 42 kudhibiti maambukizi ya Covid 19

Uganda imefunga shule zote pamoja na taasisi za elimu ya juu kwa siku 42 kufuatia wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona. Nchi hiyo ilifunga shule zote mwezi Machi 2020, na kuzifungua kwa awamu tangu mwezi Oktoba. Lakini wanafunzi wa shule za msingi na upili walikuwa hawajarejea wote shuleni.

Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumapili, Rais Yoweri Museveni alisema waalimu wote sasa watahitajika kuchanjwa kabla ya kuruhusiwa kurejea kazini.

Walikuwa wamejumuishwa katika kundi la kwanza la watu walioshtahili kuchanjwa wakati nchi hiyo ilipozindua kampeni ya chanjo ya corona mwezi Machi mwaka huu. Mikusanyiko yote ya kisiasa imesitishwa isipokuwa mikutano ya bunge na mahakama. Mikusanyiko ya umma pia imesitishwa kwa siku 42. Ni watu 20 watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi au mazishi. Usafiri wa umma na wa kibinafsi kutoka kutika wilayani kuingia jiji kuu la Kampala zitapigwa marufuku kuanzia tarehe 10 mwezi Juni. Magari ya kusafirisha mizigo hayataathiriwa na marufuku hiyo. Shughuli nyingi za kiuchumi zitaendelea kama kawaida lakini hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corono zitaimarishwa.

Nchi hiyo imethibitisha ongezekola hali ya juu ya maambukizi ya corona katika wiki mbili zilizopita ikilinganishwa na miezi iliopita. Jumla ya watu 1259 wamethibitishwa kuambukizwa, kiwango cha juu zaidi kurekodiwa tarehe 4 Juni tangu janga la corona lilipoatangazwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents