Habari

Ugiriki yakabiliwa na joto kali

Ugiriki inaendelea kukabiliwa na wimbi hatari la joto wakati wazima moto wakiendelea kupambana na moto uliosababishwa na ukame katika maeneo mbalimbali.

Kulingana na kituo cha habari cha serikali angalau watu 16 walazimika kutibiwa katika hospitali kwenye rasi ya Peloponnese, kusini mwa Ugiriki kutokana na matatizo ya kupumua.

Nyumba kadhaa katika eneo la mji mdogo wa Egion ziliharibiwa. Na kufikia leo asubuhi moto huo ulikuwa umedhibitiwa.

Hata hivyo kikosi cha ulinzi wa raia kimeonya kuwa hatari ya moto inabaki juu kutokana na ukame.

Huku hayo yakiarifia matetemeko mfululizo ya ardhi yametikisa Visiwa vya Dodecanese kusini mashariki mwa Bahari ya Aegean nchini Ugiriki.

Hata hivyo hakukuwa na ripoti za uharibifu wa mali au majeruhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents