Ugomvi wa Diamond na Willy Paul huko Kenya,Eric Omond anachuki?
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la Willy Paul na Diamond lililotokea nchini Kenya.
@el_mando_tz anasema Willy Paul alipata wasiwasi Diamond kupanda kabla yake ingemharibia yeye huenda angefanya Show mbaya kwa sababu ya nguvu ya Diamond.
Kosa la kwanza kwa Willy Paul ni hilo na hakutumia njia sahihi kuwasilisha malalamiko yake kwa waandaji wa Tamasha hilo.
Kosa la pili la Willy Paul alimlaumu Diamond wakati Diamond sio mpangaji wa Ratiba, Diamond alipangiwa ratiba kama yeye alivyopangiwa Ratiba hivyo angetakiwa kuwalaumu waandaji na Sio Diamond.
Kosa la Tatu la Willy Paul alianza kueneza Chuki kwa Wakenya kumchukia Diamond na wasanii wa Tanzania kisa kupewa Treatment ya VVIP wakati wanastahili.
Asilimia kubwa ya wasanii wa Kenya wanataka kunilinganisha na Wasanii wa Tanzania licha ya kuwa wamepitwa kwa asilimia kubwa sana.
Willy Paul angetakiwa kushirikiana zaidi na Wasanii wa Tanzania kama anataka awe mkubwa kimuziki na sio kueneza Chuki ambazo zitamfanya achukiwe zaidi.
Moja ya kitu alichojiharibia ni kwamba waandaaji wengi wa Shows au Matamasha wataanza kumkataa kumualika kwa sababu ya ugomvi wake.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive
Cameraman & editor @samirkakaa