HabariSiasa

Uingereza: Maelfu ya wafanyakazi wa reli wagoma

Maelfu ya wafanyakazi wa reli nchini Uingereza wameanza mgomo wao leo. Kiasi wafanyakazi 40,000 wanaofanya kazi ya usafi, matengenezo, watoa ishara na wafanyakazi wa vituoni wanafanya mgomo wa saa 24, huku migomo mingine miwili ikipangwa kufanyika Alhamisi na Jumamosi.

Mtandao wa usafiri wa reli wa Uingereza umekwamishwa na mgomo huo unaoelezwa kuwa mkubwa kabisa katika sekta ya usafiri katika kipindi cha miongo mitatu. Huduma za usafiri wa treni za chini ya ardhi zimeathiriwa na mgomo huo.

Vituo vikubwa vya treni havikuwa na watu mapema asubuhi huku asilimia 20 tu ya treni za abiria zikipangwa kufanya kazi.

Mgomo huo umesababishwa na mgogoro kati ya serikali na wafanyakazi wanaodai mishahara, mazingira mazuri ya kufanyia kazi na usalama wa nafasi za ajira huku shirika la reli la Uingereza likijizatiti kujikwamua kutokana na athari za janga la corona.

Related Articles

Back to top button