Habari

Uingereza na mdororo wa kiuchumi

Takwimu mpya zilizochapishwa leo zinaonesha uchumi wa Uingereza ulianguka kwa asilimia 0.2 katika robo ya tatu ya mwaka 2022 hali inayothibitisha kuwa taifa hilo limetumbukia kwenye mdodoro wa kiuchumi.

Taarifa hizo zimetolewa ikiwa ni wiki moja tangu Benki Kuu ya nchi hiyo kutoa hadhari kwamba uchumi wa Uingereza unaelekea kudorora katika wakati umma unapambana na kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei wa kiwango cha juu.

Waziri wa fedha wa Uingereza Jeremy Hunt amesema takwimu hizo mpya zinaashiria hali itazidi kuwa ngumu na serikali ya nchi hiyo italazimika kuchukua maamuzi magumu kurejesha utulivu wa kiuchumi.

Wiki inayokuja serikali ya waziri mkuu Rishi Sunak inatazamiwa kutangaza bajeti mpya ambayo kiongozi huyo anatumia itasaidia kuleta uthabiti wa kisiasa na kiuchumi baada ya mtikisiko wa wiki za karibuni ndani ya utawala wa taifa hilo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents