Uingereza wanaondoa masharti ya Corona, kuvaa barakoa na kukaa mita moja havitakuwepo (+ Video)

Waziri mkuu, Boris Johnson, alisema alitarajia kupunguza sheria za Covid -19 katika wiki mbili kutokana na kufanikiwa kwa mpango wa chanjo. Uvaaji wa barakoa na kukaa mbali zitaondolewa miongoni mwa sheria za lazima katika mwisho wa mpango wa ”lockdown” ya corona, amethibitisha Waziri Mkuu Boris Johnson.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Sir Keir Starmer, aliishutumu serikali kwa kile alichodai ni kuzembea uongozini. Sheria ya watu sita ndani ya nyumba itaondolewa na muongozo wa watu kufanya kazi nyumbani kwa miezi 16 itaondolewa.

Wazir Mkuu Boris Johnson amesema anatarajia hatua za mwisho zitaendelea kuanzia tarehe 19 Julai kama ilivyopangwa. Hii itathibitishwa tarehe 12 Julai baada ya tathmini ya data za hivi karibuni kuhusu corona.

Wakati huo huo chama kikuu cha upinzani cha Uingereza kimeishutumu serikali kwa kutowajibika, baada ya kuthibitisha mipango ya kuondoa masharti mengi dhidi ya Corona nchini Uingereza.

Uingereza ni nchi ya kwanza kufanya hivyo wakati maambukizi yakizidi kuongezeka. Bw Johnson amesema hata baada ya kuondolewa kwa sheria ya kuvaa barakoa binafsi ataendelea kuvaa yake katika maeneo yenye watu wengi kama ” adabu’’ .

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CQ-pL0ojkpu/

Related Articles

Back to top button