Habari

Ujenzi wa hospitali ya Muhimbili utaogharimu Tsh Bil. 600 (Picha+Video)

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) @shakazulu36 amefanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo akiwa kwenye ziara hiyo amepata nafasi ya kupokea taarifa zinazohusu taasisi hizo.

Shaka ameeleza mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya afya huku akizungumza mipango ya kuijenga Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo zaidi ya Sh.bilioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo ambao unakwenda kuandika historia nyingine katika sekta ya afya nchini.

Hata hivyo amewapongeza watoa huduma katika taasisi hizo kutokana na huduma bora ambazo wanazitoa katika kuwahudumia Wananchi huku akieleza kwamba Kuna mambo makubwa na mazuri yamefanyika tofauti na baadhi ya watu wanavyozungumza.

Related Articles

Back to top button