AfyaHabari

Ujerumani kuhalalisha bangi

Ujerumani imefungua njia ya kuelekea kuhalalisha ununuzi na umiliki wa kiasi kidogo cha bangi kwa ajili ya starehe.

Watu wataruhusiwa kununua kiasi kisichozidi “gramu 20 na 30” za bangi kwa matumizi yao binafsi. Sheria hiyo hata hivyo itahitaji kupasishwa na Umoja wa Ulaya na bunge la Ujerumani kabla ya kuanza kutekelezwa mnamo mwaka 2024.

Hatua hiyo imezusha mjadala mkubwa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, huku wakosoaji wakiibua wasiwasi kwa afya ya umma.

Waziri wa Afya wa Ujerumani Karl Lauterbach amesema kulingana na rasimu hiyo, uzalishaji na usambazaji wa bangi utaruhusiwa katika mfumo ulioidhinishwa na unaodhibitiwa na serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents