HabariSiasa

Ujerumani: Wawili wathibitishwa kuwa na homa ya Nyani

Mamlaka nchini Berlin imesema kuwa takriban watu wawili wamethibitishwa kuambukizwa homa ya nyani.

Ugonjwa huo wa nadra unaoambukiza na ambao husababisha upele lakini usiokuwa na athari kubwa, hupatikana zaidi katika sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi.

Katika wiki za hivi karibuni, zaidi ya visa 130 vilivyothibitishwa au kushukiwa kuwa vya ugonjwa huo viimerekodiwa barani Ulaya.

Virusi hivyo pia vimeenea hadi Marekani, Canada, Israel na Australia. Shirika la Afya Duniani WHO limesema visa vingi vya awali vina uwezekano kwamba viliambukizwa kingono na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume.

Gazeti la El Pais limeripoti kwamba mamlaka ya Uhispania inachunguza ikiwa tamasha la fahari ya mashoga kwenye kisiwa cha kitalii cha Gran Canaria ndio chanzo cha maambukizo kadhaa.

Vyombo vya habari vimeripoti jana kuwa kufikia sasa, Uhispania imethibitisha visa 30, huku zaidi ya visa 39 vikishukiwa kuwa vya ugonjwa huo.

Virusi hivyo vya ugonjwa wa nyani husababisha homa, maumivu ya mwili, baridi na uchovu kwa wagonjwa wengi lakini vinaweza kusababisha upele kama vile tetekuwanga na vidonda kwenye mwili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents