Ujumbe wa Mo Dewji baada ya kifo cha Hanspope

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa:- “Moyo wangu una maumivu makali sana. Bado ni vigumu kuamini na kukubali kuwa mjumbe wetu, kaka yetu, Zakaria Hans Poppe hatunaye tena.

Kaka yangu, nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele. Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee, na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na maslahi binafsi. Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na wasioitakia mema Simba.

Kaka yangu, Umetangulia nasi tutafuata. Nitakukumbuka sana kaka yangu. Natoa pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na wanafamilia wote na mashabiki wa Simba kwa kumpoteza ndugu yetu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.πŸ™πŸΎπŸ•ŠοΈ#RIPZHP
//
My heart is in pain and broken. It is still hard to accept that our board member, Zakaria Hans Poppe is no longer with us.

My brother, I have worked with you for many years, and each day you put Simba’s interests first. My brother, you were kind in a special way, you were straight forward when it came to defending Simba, not because of your own interests. You were a friend of the friends of Simba and you were against all those who never wanted good for Simba.

My brother, you have left us now, but we will follow you. I will miss you my brother. My condolences to his family, relatives, friends and the whole Simba family and fans for the lost of our dear one. May God rests his soul in eternal peaceπŸ™πŸΎπŸ•ŠοΈ

Related Articles

Back to top button