Siasa

Ujumbe wa Zitto kwa Membe: Umefukuzwa uanachama CCM, bado unatetea haki yako unganisha nguvu vyama mbadala

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganishe nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.

Kushoto ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na kulia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Juni 30, 2020, ambapo imeandikwa hivi,

“Ndugu yangu Bernard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM, ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala” umeeleza ujumbe huo ambao umetolewa na Zitto Kabwe.

https://twitter.com/ACTwazalendo/status/1277941872070139905

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents