Habari

Ukame wa kutisha waikumba Pembe ya Afrika

Ukame wa kutisha unaoikumba Pembe ya Afrika, mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40, huenda ukawa mbaya zaidi, kulingana na uchambuzi wa hivi punde kutoka kituo cha utabiri wa hali ya hewa cha kikanda cha jumuiya ya Maendeleo ya ukanda wa Afrika Mashariki (IGAD).

Msimu wa mvua ambao huanza mwezi Oktoba hadi mwezi Desemba ni muhimu sana kwa Pembe ya Afrika. Kwa kawaida huleta hadi 70% ya mvua kwa mwaka katika baadhi ya maeneo, kwa mfano mashariki mwa Kenya.

Lakini utabiri ni mbaya tena: mvua zitachelewa na zitanyesha kwa kiwango kidogo.

“Hali hii inatokana na kile tunachokiita Pande mbili za Bahari ya Hindi, jambo ambalo husababisha kupoa kwa eneo la bahari karibu na ukanda wetu. Kwa ujumla huleta mvua ndogo kuanzia mwezi Oktoba hadi mwezi Desemba.

Hili pia linahusishwa na kimbunga Niña katika Pasifiki ambayo tayari imekuwa ikiendelea tangu mwaka jana na ambayo itaendelea, “amebainisha Eunice Koech, mchambuzi katika kituo cha hali ya hewa cha kikanda cha IGAD.

Fedha zaidi kwa ajili ya kuzuia

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yanahofia athari za msimu huu wa tano wa mvua kukosa katika uzalishaji wa kilimo na mifugo, wakati uhaba wa chakula tayari unafikia viwango vya kutisha.

“Bila shaka kutakuwa na athari kwa malisho na rasilimali za maji, lakini pia katika uzalishaji wa chakula. Baadhi ya mazao yanayokua haraka hulimwa katika msimu huu. Yote haya yanafanya hali kuwa mbaya zaidi,” anaonya Ahmed Amdihun, anayesimamia idara ya kudhibiti majanga katika IGAD.

Ahmed Amdihun anatoa wito kwa serikali za eneo hilo kuongeza misaada ya kibinadamu lakini pia kutoa fedha zaidi katika kuzuia ili kusaidia jamii hizi, idadi ya watu walioathirika zaidi, kukabiliana na ukame huu, ambao unatazamiwa kuongezeka.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema lina wasiwasi mkubwa kuhusu hali hii, kwani watu 700,000 tayari wako katika hatari ya njaa katika baadhi ya maeneo ya Ethiopia na Somalia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents