Burudani

Ukinizingua nakuzingua – Diamond Platnumz (Video)

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema yeye ni binadamu mvumilivu mno tofauti na watu wanavyomfikiria.

Diamond amesema watu wengi wanahukumu maisha yake bila kujua uhalisia akisema maisha yake ya mtandaoni ni ya tofauti na maisha halisi na wale wanaomfahamu wanalifahamu hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha Tamasha la Muziki litakalofanyika April 26, 27 Viwanja vya Posta Dar es Salaam msanii huyo amesema sio rahisi kwa wengine kuyastahimili anayopitia.

“Kuna watu walikuwa wanasema tatizo Diamond akisemwa au akikosolewa anakasirika Sheikh…… Mimi ndio mtu ninaongelewa kwa maneno tofauti kuliko yeyote katika hili Taifa, ushawahi kuniona nimejibizana hata siku moja, moyo wangu nikikupa mimi unaweza kudondoka ……. nikikupa sasahivi ……ukifika hapo nje unadondoka Puuuuhhh!

“Miongoni mwa wasanii ambao ni wakomavu, shupavu ni mimi, wewe andika sema chochote unachokitaka, sikujibu, siterereki sanasana nikiona umezidi nitakutumia tuu barua,, eehn bhana  usinizungumzie imetosha, sikupeleki polisi wala sikudai Hela amesema Diamond Platnumz.

Diamond amedai kuwa wasanii mbalimbali watatumbuiza kwenye Tamasha hilo kutoka ndani na nje ya Nchi watatumbuiza kwenye Tamasha hilo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents