FahamuHabari

Ukraine yaidungua droni yake yenyewe katikati ya jiji la Kyiv

Vikosi vya Ukraine vimeidungua ndege yake isiyokuwa na rubani ambayo ilisema kuwa ilikuwa imepoteza udhibiti juu ya eneo la katikati mwa mji mkuu Kyiv.

Kulikuwa ni milipuko ya dakika 15 hadi 20 siku ya Alhamisi jioni huku mifumo ya ulinzi ya anga ikijaribu kuidungua katika eneo lililopokaribu na ofisi ya rais.

Mkuu wa wafanyakazi wa ofisi ya rais nchini Ukraine Andriy Yermak awali alisema kuwa ilikuwa ni droni ya adui ambayo ilidunguliwa.

Lakini jeshi baadaye lilikiri kuwa ilikuwa ni droni ya Ukraine na iliangamizwa ili kuepuka “hali zisizohitajika”.

Katika taarifa yake, ilisema Bayraktar TB2 UAV [chombo cha anga kinachojiongoza] kilikuwa kimepoteza udhibiti majira ya saa mbili usiku kwa saa za eneo(17:00 GMT) katika jimbo la Kyiv , wakati wa safari iliyopangwa.

Iliongeza kuwa ilichukua uamuzi wa kuidungua “kwani uwepo wa UAVs kwenye anga la mji mkuu bila udhibiti inaweza kusababisha athari zisizohitajika”.

Hapakuwa na wahanga au majeruhi kutokana na kuangua kwa droni, ilisema taarifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents