Habari

Ulaya wapata mashaka timua timua ya wafanyakazi Twitter

Umoja wa Ulaya jana umeleezea wasiwasi kuhusu upunguzwaji wa wafanyazi katika kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter, tangu ilipochukuliwa na tajiri Elon Musk.

Hii imefuatia ripoti za kufungwa kwa ofisi ya uraghibishi ya kampuni hiyo mjini Brussels.

Kamishna wa sheria ya Umoja wa Ulaya Didier Reynders aliwambia waandishi habari mjini Dublin, ambako Twitter na kampuni nyingine za teknolojia za Marekani zina makao yake makuu ya Ulaya, kwamba wana wasiwasi kuhusu uamuzi wa kupunguza zaidi na zaidi idadi ya watu wanaofanya kazi kwenye kampuni hiyo.

Reynders aliezea wasiwasi huo baada ya mkutano na wawakilishi wa Twitter, walimojadili suala la matamshi ya chuki, ambapo alisema majadiliano kama hayo yanahitaji kuwa na rasilimali watu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents