
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ya Gridi ya Taifa kuanzia majira ya saa 8:22 hivyo kusababisha baadhi ya maeneo chini kukosa huduma ya umeme.
Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurejesha huduma.
Shirika linawaomba uvumilivu wateja wake katika kipindi hiki ambacho huduma ya umeme inakosekana.