UNICEF kukutana na wabunge Desemba 11 Dodoma

KATIKA kuadhimisha miaka yake 75 ya kazi katika kushughulikia masuala mbalimbali ya watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto, UNICEF litakutana na wabunge Desemba 11 jijini Dodoma.

Shirika hilo limefanya kazi katika kusaida watoto kwenye nyanja mbalimbali za elimu, afya, ustawi wa jamii na masuala mengine mtambuka.

Katika kuungana na shirika hilo kusherehekea miaka yake 75 wadau wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii ya kuungana na shirika hilo katika kujadilia namna ya kushiriki katika kuimarisha mustakabali wa maisha bora ya watoto.

Kati ya mambo yanayojadiliwa kwa maisha ya watoto ni pamoja na suala zima la mabadiliko ya tabia nchi ambapo jamii imetakiwa kulinda mazingira ili kujenga maisha bora yenye mazingira salama kwa kizazi cha sasa na kijacho ili kisije kuishi katika mazingira yasiyo salama.

Hashtags:

#UNICEF75
#KwaKilaMtoto
#ForEveryChild

Related Articles

Back to top button