AfyaHabari

Unijua sababu ya dawa ya Mkongo kupigwa marufuku Tanzania?? soma hapa

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo kwa binadamu, na kwamba tayari limekwishaifutia usajili baada ya kubaini imechanganywa na dawa za kuongeza nguvu za kiume (Viagra).

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo hii leo Julai 27, 2022, mkoani Morogoro, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema baraza katika uchunguzi wake, limebaini dawa hiyo ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala, na kwamba kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki ambaye ni Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents