United yajipanga kumuuza Pogba, tetesi zote za soka Ulaya hizi hapa

Manchester United wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, kabla ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu huu. (Star)

Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers anapigiwa upato kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer kama meneja wa Manchester United. (Eurosport)Aaron Ramsey

Everton na Newcastle United wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey, 30. (Goal

Nyota wa Barcelona wamechukizwa na kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho,

wakimshutumu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa kuzembea huku kukiwa na tetesi za kuhamia Newcastle United. (Star)

Manchester United wana matumaini ya kuishinda Chelsea katika harakati za kumsajili mlinzi wa Ufaransa wa miaka 22- Jules Kounde kutoka Sevilla. (AS via Express)

Liverpool wanamtaka winga wa West Ham Muingereza Jarrod Bowen, 24, lakini watamnunua mwezi Januari. (Mirror)Jules Kounde

Kocha wa Genoa Andriy Shevchenko anataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 23. (Secolo XIX – in Italian)

Newcastle United huenda wakampata Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bila malipo ikiwa winga huyo atakataa kusaini mkataba mpya na Barcelona. (Express)

Barcelona wanajiandaa kumpatia Dembele ofa ya mkataba ambayo inahusishwa na muda atakaokuwa uwanjani. (Sport)Ousmane Dembele

Barcelona huenda wakamsaini tena mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, mwaka 2023 wakati mkataba wake na Paris St-Germain utakapomalizika, anasema mgombea wa urais wa zamani wa klabu hiyo Victor Font. (Marca)

Newcastle United wameanza kufanya mazungumzo na wawakilishi beki wa Bayern Munich na Ujerumani Niklas Sule,26. (Newcastle World)

Klabu ya Ujerumani Borussia Monchengladbach inatafakari uwezekano wa kuwasilisha dau la kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 22. (Sun)Eddie Nketiah

Giovanni Simeone, mwana wa kiume wa kocha wa Atletico Madrid Diego, ni wa kwanza kwenye orodha ya washambuliaji wanaosakwa na West Ham. Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina wa miaka 26 kwa sasa anachezea klabu ya Serie A ya Verona, kwa mkopo kutoka Cagliari. (Express)

Kocha wa zamani wa Marekani na Swansea City Bob Bradley, 63, anajiandaa kuwa meneja wa Toronto FC. (AS)

Related Articles

Back to top button