Habari

Upinzani Guinea wahimiza jeshi kufanikisha uchaguzi

Kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini Guinea, Cellou Dalein Diallo ameutaka uongozi wa kijeshi nchini humo kuunda serikali ya mpito na kutangaza muda wa kufanyika uchaguzi baada ya mapinduzi ya juma lililopita.

Diallo amesisitiza kuwa jeshi kwa sasa lazima lithibitishe nia yake ya kurejesha mamlaka kwa raia kama walivyoahidi wakati mapinduzi dhidi ya rais Alpha Conde Septemba 5.

Diallo anamshutumu rais Conde aliyeondolewa madarakani kwa kujiangamiza mwenyewe baada ya kuwa na fikra ya muhula wa tatu madarakani kwa kusema ukomo wa madaraka kikatiba hauna nafasi kwake.

Akizungumza katika mahojiano yake na shirika la habari la AP, Diallo amesema Conde amekisaliti kiapo chake na kuliingiza taifa katika mgogoro mkubwa na kumwelezea mpinzani wake huyo wa muda mrefu kama dikteta.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents