Ushauri kwa Yanga kama wanataka kuifunga Tanzania Prisons (+Video)

Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Abbas Pira amewataka Yanga SC kuhakikisha wanapambana dakika 20 za mwanzo kupata walau goli mbili dhidi ya Tanzania Prisons kama wanahitaji matokeo mbele ya vijana hao.

Pira ambaye amewahi kufanya majaribio ya mpira wa kulipwa katika klabu ya Chelsea pale England amewahasa Wananchi hao hasa akizingatia uwezo na aina ya mpira wanaocheza wapinzani wao Tanzania Prisons.

Kikosi cha Wananchi kitashuka kwenye Uwanja wa Nelson Mandela majira ya saa 10:00 alasiri kuwakabili Tanzania Prisons kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Related Articles

Back to top button