Ushirikiano na wanahabari,Ubunifu ndio nyenzo ya ufanisi-Msigwa

Mkurugenzi wa Idara ya Habari  na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewataka maafisa habari za wizara zote kuimarisha mahusiano na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Msigwa ametoa maelekezo hayo jana jijini Dodoma katika mkutano wake na  Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara zote kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali vile vile njia ya kuboresha vitengo hivyo katika utoaji wa taarifa za Serikali.

Msigwa ameagiza wakuu hao wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutafuta namna nzuri za kushirikiana na vyombo vya habari kuimarisha mahusiano baina yao ili iwe rahisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Vile vile Mkurugenzi Msaidizi (Mawasiliano Serikalini) wa Idara hiyo, Zamaradi Kawawa amewataka maafisa hao kuimarisha mahusiano na wadau wao wote.

“Tuwe na mahusiano mazuri kati  yetu, na watumishi wenzetu wa wizara zetu na wizara nyingine,

Mwaka 2005 Serikali ilianzisha Vitengo vya Mawasiliano Serikalini na mwaka 2016 Serikali ikapitisha Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ili wanahabari na wananchi wapate taarifa za utendaji kazi unaofanywa na Serikali.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button