Utajisikiaje ukigundua ulikuwa unalala na nyoka wengi kitandani kwao (+Picha)

Mwanamke mmoja nchini Marekani amekutwa na mshuto mkubwa baada ya kugundua nyoka 18 waliokuwa wakiishi chini ya kitanda chake.

Trish Wilcher aliogopa sana wakati alipoona familia ya nyoka hao kitandani kwake waliokuwa wakiishi kwenye chumba chake cha kulala huko Augusta, Georgia nchini Marekani.

Trish alituma picha katika mtandao wa facebook na kusema kuwa “Angalia nyoka wote hawa waliopo katika chumba changu cha kulala. yaaani nimechanganyikiwa.”

Trish na mumewe Max waligeuza kitanda chao cha kulala yaani “juu chini” kuangalia kuna nini, Waliishia kupata watoto 17 wa nyoka na mama yao.

Trish alisema anaamini kwamba nyoka hao waliingia ndani ya nyumba yake kwa sababu ardhi iliopo karibu na nyumba yao ilikuwa inafanyiwa matengenezo na hivyo nyoka hao wakakimbilia nyumbani kwake.

Related Articles

Back to top button