
Siku ya leo viongozi wa Timu ya Mpira wa Kikapu nchini ya @pazibasketball wamefanya mazungumzo na Wandishi wa Habari kuelekea safari yao ya kwenda Afrika kusini kwa ajili ya mashindano ya
AFRICA BASKETBALL LEAGUE ambapo walifuzu.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Msemaji wa Timu hiyo @officialbabalevo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwekeza kwenye timu hiyo
ili kusaidia kukuza mchezo wa mpira wa kikapu
Tanzania.
Lakini pia ameongea mchezaji wa timu hiyo @hasheemthedream , kocha wa timu hiyo na Kiongozi wa Bodi ya Ligi.