Habari

UTEUZI: Rais Samia amteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Mbunge

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Tax ameteuliwa kutoka kwenye nafasi kumi za Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Tax alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti, 2021.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents