Michezo

Uwanja wa Fainali ubadilishwe – Haji Manara (Video)

Kwa kilichotokea Arusha last weekend kinatupaswa kukifanya kama funzo,Semi final tu Washabiki walimwagika hadi wengine kukosa nafasi ya kuingia Uwanjani na hatimae kusababisha fujo.

Ikumbukwe ilikuwa ni Sheikh Amri Abedi,Now tunakwenda kwenye fainali yenyewe ya Kombe la Shirikisho,tunaipeleka Babati Manyara, kiwanja chenyewe kina jukwaa moja tu, wataalamu wanasema capacity yake haifiki washabiki elfu tatu hadi elfu nne, Swipe uuone uwanja wenyewe katika picha.

Mamlaka zetu nawashauri kwa heshma kubwa ondoeni mechi pale kwa kuwalinda Washabiki,Babati ni Centre ya mikoa kadhaa inayoizunguka,,Watu watatoka katika mikoa tofauti kuja kuona fainali na Yanga yao,Team hii ya Wananchi haijawahi kucheza huko toka iumbwe,imagine hamu ya Wanazi wetu kuiona Team yao,fikirieni na udogo wa uwanja,tunaweza kuepuka maafa kwa kuipeleka fainali sehemu nyingine.

Kwa sisi watu wa Events na Promotions huwa tunazingatia vitu kadhaa kabla ya tukio husika,
π—™π—”π—–π—œπ—Ÿπ—œπ—§π—¬, π—–π—”π—£π—”π—–π—œπ—§π—¬, π—–π—’π—‘π—œπ—©π—‘π—˜π—‘π—–π—˜ 𝗑𝗔 π—Ÿπ—’π—šπ—œπ—¦π—§π—œπ—–π—¦.

Kwa Tukio kubwa la fainali kupeleka hapo hatukuzingatia mambo hayo, najua pamoja na nia nzuri ya kuusambaza mpira maeneo mengi ya nchi lakini uwanja wa Babati haujawa tayari kuhost fainali hii kubwa,,

Wenzetu kote duniani fainali ya Makombe kama haya huchezwa katika Main Stadimu ya Nchi na hata Mgeni rasmi huwa kiongozi mwandamizi wa nchi,kwa nchi za kifalme lazma aje Royal family kukabidhi kombe.

By the way kibiashara pia sio sahihi kama tunataka tuumarket mpira wetu ndani na nje ya nchi,Imagine makampuni makubwa ya nje yakiona fainali katika uwanja kama huu watatuonaje? Watapata hamu ya kuja kuinvest kwenye mpira wetu?

Nini nafasi yaΒ @azamtvtzΒ katika eneo la Production? Wanajisikiaje kurusha mechi ya fainali pale ?Sponsor CRDB mileage gani watapata kwa fans wachache?

Ahhh pengine mawazo yangu leo yanaweza kuwa sio sahihi lakini nimeandika haya ili yasitokee tusiyoyataka na kuyatarajia, tuna AFCON mbele ya safari kama Host, tusije kuonekana hatuko tayari kuandaa,tusiwape nafasi maadui wa nchi yetu kisa siasa zetu.

Ahhhh,Niko tayari pia kukosolewa kwa hoja sio kunitazama mtoa hoja ni nani.

 

https://www.instagram.com/p/C7OYXkkNKas/

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents