Habari
UWT wamuonya Mwenyekiti Tundu Lissu

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) umesema utapambana na chama chochote ama mtu yeyote atakayeeneza kile ilichokiita dhihaka ama propaganda ovu dhidi ya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UWT taifa, Mary Chatanda Jumanne Februari 4,2025 jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Wanawake kuelekea maadhimisho ya Miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema UWT ni jeshi kubwa hivyo mtu yeyote atakayetaka kupambana na Rais Samia ajipange, na amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia lugha za staha wanapotaka maridhiano kwa jambo lolote na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.