Burudani

Vanessa Mdee ashirikishwa na producer wa nyimbo 2 kwenye album ya Beyonce (Lemonade) Diplo (Major Lazer)

Vanessa Mdee anaendelea kwenda Juu. Fresh kutoka kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Gidi jijini Lagos, Nigeria wikiendi ya Pasaka, Cash Madame huyo ameonekana kuingia location kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na kundi la watayarishaji wa muziki, Major Lazer linaloongozwa na Dj wa Marekani, Diplo.


Vanessa Mdee akiwa na Diplo

Kwenye wimbo huo pia member wa Major Lazer, Mmarekani mwenye asili ya Jamaica, Walshy Fire ameshiriki na kuufanya kuwa mradi wa Major Lazer ft. Vanessa. Diplo na Walshy Fire nao walitumbuiza kwenye tamasha la Gidi.


Vanessa na Walshy Fire

Vanessa ameshare picha kwenye Instagram akiwa location na watayarishaji hao na kuandika, WORLDWIDE ???????????? x ???????? x ???????? @diplo @walshyfire Happy Easter ???? #MajorLazer #VeeMoneyIfYouNasty.”

Naye Diplo amepost picha kwenye akaunti yake yenye followers milioni 3.5 na kuandika, US to TZ @vanessamdee.”

Major Lazer linaundwa na members watatu, Diplo, Jillionaire, na Walshy Fire. Ilianzishwa na Diplo na Switch, lakini Switch alijiondoa mwaka 2011.

Lakini ni Diplo ndiye mwenye jina kubwa zaidi kwenye kundi hilo na ameshiriki kutengeneza hits za wasanii wengi wakubwa. Kwenye album ya Beyonce, Lemonade, Diplo ametayarisha nyimbo mbili, Hold Up na All Night.

Diplo anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 26. Major Lazer kumshirikisha Vanessa ni nyundo ya mwisho inayompeleka Vee Money kimataifa moja kwa moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents