Video: Alikiba anaizimia Kwetu ya Raymond, mtazame akiimba

Pamoja na kutoendelea kupikika chungu kimoja na Diamond, Alikiba hana tatizo na vijana wake wa WCB. Na ndio maana ni shabiki mzuri wa nyimbo zao, hususan Kwetu wa Raymond.

Video inayomuonesha hitmaker huyo wa Aje akiuimba wimbo huo wa Ray Vanny, imesambaa mtandaoni na kusababisha mjadala chanya. Wengi wamempongeza Kiba kwa kuonesha kutochukia boga na maua yake. Na hakika wimbo huo anaonesha kuupenda kweli kweli. Mcheki hapo juu.

Ray naye amewahi kuonesha dalili za kuwa haoni tatizo siku moja akija kufanya wimbo na Kiba na kwamba hata wakikutana wanaongea vizuri kabisa.

“Alikiba huwa nikikutana naye napiga naye stori, tunasalimiana tunacheka, ananiambia kuwa nafanya kazi nzuri, hatujawahi kuongea sana,” Ray aliwahi kukiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Aliongeza, ” Ikitokea siku naweza kufanya naye kolabo kwasababu ‘end of the day’ wote tunafanya muziki ni biashara pia, mashabiki wetu wanapenda kuona ‘combination’ za watu tofauti tofauti, hata nikikutana naye hatufungiani vioo.”

Hii ni nzuri!!

Related Articles

Back to top button