Burudani

Video: Ben Pol aigiza mbwia unga kwenye filamu ya ‘Sunshine’

Ben Pol ataonekana kama mhusika mkuu kwenye filamu mpya iitwayo ‘Sunshine’ inayotarajia kutoka mwezi February mwaka huu. Kwenye filamu hiyo, Ben Pol amecheza kama kijana asiyependa kazi na anatumia madawa na kulevya pamoja na ulevi.

Akizungumza na Bongo5, Ben Pol amesema ‘Sunshine’ ni filamu inayoelezea maisha ya vijana halisi Wakitanzania ambao hawataki kazi.

“Sunshine ni filamu ambayo imeandaliwa na Karabani,mimi nimecheza kama mhusika mkuu ambaye nalipwa.Filamu hii itazinduliwa mwaka huu mwezi wa pili ingawa sasa hivi inaonyeshwa DSTV channel 158. Mimi nimecheza kama kijana ambaye naishi na mama pamoja na dada yangu,ila mama anakuwa ananitetea katika mambo mengi ila dada yangu hapendi nijihusishe na madawa ya kulevya pamoja na pombe,” amesema Ben Pol.

Related Articles

Back to top button