Burudani

Video: Marioo aweka rekodi ya wimbo ulioangaliwa zaidi YouTube nje ya WCB, 2022

Muziki wa BongoFleva kwa sasa unasherekea mafaniko ya ukuwaji wa wasanii wapya ambao uwezo wao unaweza kushindanishwa na wasanii ambao walitawala muziki huo kwa muda mrefu.

Hawa ni wale wasanii ambao ngoma zao zilikuwa zinagonga views nyingi kutokana na ngoma zao kufanya vizuri kupitia platform za mitandao kama YouTube na mitandao mingine yakuuza nyimbo.

Kwa sasa Marioo ameuthibitishia umma uwezo wake kwa kuvunja rekodi ambazo zilikuwa zifanywa na wasanii wa WCB, King Music na Konde Gangs.

Wimbo wake  wa ‘Mi Amor’  akiwa na Jovial ambao umetimiza mwaka mmoja kwa kufikisha Views Milioni 23 YouTube rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na msanii yeyote nje ya lebo ya WCB na King Music.

Wimbo mwingine wa Marioo uliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja kupitia rekodi hiyo ni wimbo wake ‘Naogopa’ akiwa na Harmonize ambapo mpaka sasa una Views Milioni 21 YouTube ndani ya mwaka mmoja pekee.

Msanii mwingine ambaye ameingia kwenye rekodi hiyo ni Jay Melody kupitia wimbo wake ‘Nakupenda’ ambao mpaka sasa una Views 21 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Maua Sama ndiye msanii kike pekee nje ya WCB na King Music anayeshilia rekodi hiyo kupitia wimbo wake Iokote akiwa na Hanstone ambao mpaka sasa wimbo huo una views 25 na ulitoka miaka 4 iliyopita.

Naye Darassa kupitia wimbo ‘Muziki’ ambao ulitoka miaka 8 iliyopita ulipata views Milioni 22 na kuwa msanii pekee ya hip hop kupitia watazamaji wengi kiasi hicho.

Wimbo pekee wa King Music ambao umepata views zaidi ya Mil 20, ni wimbo wa Alikiba ‘Mwana’ ambao una Views Milioni 30 na ilitoka miaka 8 iliyopita.

Wimbo wakushirikiana wa Innoss’B na Diamond Platnumz Yope Remix ndio wimbo wa muziki ulioangaliwa zaidi YouTube ukiwa na Views Milioni 205 kwa kipindi cha miaka 3.

Kwa upande wa Konde Gang, wimbo pekee ambao uliweza kufikisha views zaidi ya Milioni 20, ni wimbo Mang’dakiwe Remix  ambao alikiwa na Dj Obza na Leon Lee ambao uliitoka mwaka 2021.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents