Video: ‘Messi ni wa Sayari nyingine, naipenda Simba, Yanga ingemwacha Zahera afanye kazi yake’- Mwakilishi La Liga

Wiki hii Bongo 5 Tv imepata bahatika ya kufanya mahojiano maalumu na mwakilishi wa ligi kuu nchini Hispania La Liga, Mr Alvaro Paya ambapo miongoni mwa mazungumzo hayo ni pamoja na utata wa muda mrefu unaoendelea kugubika vichwa vya habari kuhusu nani ni mchezaji bora duniani kati ya viumbe hawa wawili Lionel Messi na Ronaldo lakini pia je endapo Catalonia litapata uhuru je hatma za klabu ya Barceloa, Espanyolna na nyingine zipoje ambazo zinapatikana kwenye jimbo hilo, zitajiondoa La Liga.

Mbali hayo lakini pia Mr Alvaro ametaja klabu ambayo kwake anazipenda kutoka Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara huku akitoa maoni yake kuhusu kutimuliwa kazi kwa kocha Mwinyi Zahera baada ya kuulizwa swali na mwandishi.

Related Articles

Back to top button