BurudaniVideos

Video: Mkenya Sarah Ikumu (15) afunika mbaya kwenye shindano la Britain’s Got Talent, apewa ‘golden buzzer’

Muimbaji mwenye miaka 15, mtoto wa wazazi wa Kenya, Sarah Ikumu anaogelea kwenye dimbwi la ustaa baada ya Jumamosi iliyopita kufunika mbaya kwenye shindano la Britain’s Got Talent.

Kuimba kwake kulimfanya awe mshiriki wa kwanza mwaka huu kupewa kitufe cha dhahabu (golden buzzer) kinachomaanisha kuwa anaingia moja kwa moja kwenye hatua inayofuata.

Sarah Ikumu ameanza kuimba kanisani tangu akiwa na miaka mitano.

Baba yake Alex Gatoto, kutoka Kenya ni mchungaji na amekuwa na mchango mkubwa katika uimbaji wake.
Wazazi wake walihamia nchini Uingereza na wanaishi Milton Keynes.

Wimbo aliouimba unaitwa And I Am Telling You na kumfanya jaji mkuu, Simon Cowell abofye kitufe cha dhahabu. Tayari mtoto huyo ni maarufu Youtube na amekuwa akipost video akiimba nyimbo ikiwemo ya Aretha Franklin, Think na Adele, When We Were Young.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents