Habari

Video: Msako waendelea kwa muuaji wa pasaka aliyempiga risasi mzee mpita njia na kuweka video ya tukio Facebook

Msako mkali unaendelea kumnasa Steve Stephens, 37 wa Cleveland, Ohia nchini Marekani, aliyehusika kwenye tukio la mauaji ya mzee wa miaka 74, Robert Godwin.

https://www.youtube.com/watch?v=N7AUvmHCF50

Muuaji huyo alidai kufanya kitendo hicho baada ya kukorofishana na mpenzi wake, na hasira zake aliamua kuzihamishia kwa mzee mpitanjia huyo huku akirekodi mauaji hayo na kuweka video Facebook.

Godwin, mfanyakazi wa zamani wa kiwandani na fundi mechanic, ana watoto 10 na wajukuu 14.

Mtoto wa kike, Tonya Godwin-Baines ameiambia CNN Jumatatu hii kuwa familia imemsamehe muuaji huyo.

“Each one of us forgives the killer, the murderer. We want to wrap our arms around him,” amesema.

Mwingine, Robert Godwin Jr. amesema, “Steve, I forgive you … I’m not happy [with] what you did but I forgive you.”

Watoto wake wamesema baba yao aliwafundisha thamani ya kazi. Aliwafundisha jinsi ya kumpenda kumpenda na kumuoga Mungu na jinsi ya kusamehe. Meya wa Cleveland, Frank Jackson ametangaza zawadi ya $50,000 kwa mtu atakayesaidia kupatikana kwa Stephens.

https://www.youtube.com/watch?v=RhPCbeSK8XM

Stephens aliweka video kwenye Facebook ikionesha akimnyooshea bastola mzee huyo aliyekuwa akikatiza tu barabarani na shughuli zake. Sekunde chache kabla ya kumpiga risasi, Stephens alimuuliza mzee huyo aseme jina la mwanamke ambaye ana ukaribu na mtuhumiwa.

“She’s the reason why this is about to happen to you,” alisema Stephens. Baada ya hapo alimpiga risasi mzee huyo aliyepoteza maisha pale pale.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents