Burudani

Video: Mwana FA aeleza alivyorudisha uswahiba wake na Hermy B

Mwana FA na Hermy B walirejea tena mwishoni kabisa mwa mwaka jana na kuungana pamoja kutayarisha wimbo ‘Asanteni kwa Kuja.’

Hiyo ilikuwa ni baada ya takriban miaka miwili waliyokaa bila kufanya kazi.

“Unajua kuna wakati mwingine haijalishi wewe na mimi hatuko poa lakini mnajikuta mko katika eneo moja pengine kwenye maisha yenu ya kila siku, starehe, kazi ama nini,” amesema FA kuhusu walivyopatana tena na mtayarishaji huyo.

“Na tukagundua kwamba in personal level hakukuwa na tatizo, nafikiri tatizo lilikuwa kwenye biashara na tatizo halikuwa la Hermy B moja kwa moja ama la kwetu moja kwa moja. Nafikiri alikuwa anajaribu kutengeneza some sort of a management ya B’Hits, sasa ikaja na sheria bila kuangalia sisi na yeye relationship yetu kwenye hiyo personal level ikoje na ndipo tulipokosana kwasababu pengine wakataka kututreat kama wengine wote, sheria zikaja kali sana mimi nikamwambia hatuwezi kufanya hivi,” ameongeza..

“Na kutengena kwa muda fulani kukafanya kila mmoja aone umuhimu wa mwenzie, kwamba kumbe nilikuwa nafikiri niko level hii lakini siko level hii bila hawa jamaa na sisi kwamba pengine tungeweza kufanya muziki wetu lakini tungeweza kufanya muziki wetu mzuri kirahisi zaidi kama tungekuwa na Hermy. So mnakuta ile position mliyokuwa nayo mnapoteza vingi kuliko mnavyogain. So ilivyofika mahali sisi na yeye hatuna tatizo, tukikutana tunakaa tunaongea huko maviwanjani, then Josh ndio akaingilia kati kwasababu naye tunahang naye everytime.”

FA anasema Josh aliwaambia kuwa haoni kama wana tatizo na wakaamua kuyamaliza na kwamba hilo lilitokea muda mrefu uliopita.

“Haikuwa process ndefu sababu hakukuwa na chuki za moja kwa moja. Nafikiri tulipishana tu na ni masuala ya biashara na binadamu lazima wapishane.”

Mwana FA amesema tayari amesharekodi takriban ngoma tatu mpya na Hermy B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents