Video: Saraha ashika nafasi ya pili kwenye nusu fainali ya mashindano makubwa ya Melodifestivalen 2016 Sweden

Saraha amekitangaza Kiswahili kwa kishindo kikubwa kwenye mashindano ya 59 ya Melodifestivalen 2016 nchini Sweden.

Muimbaji huyo aliingia kwenye nusu fainali na kutumbuiza wimbo mpya uitwao ‘Kizunguzungu.’ Kutokana na wimbo huo, Saraha alishika nafasi ya pili.

Kama angeshinda angesonga mbele kushiriki shindano la Eurovision Song Contest 2016. Hata hivyo wimbo wake huo umeongoza kwenye mtandao wa iTunes.

Nusu fainali hiyo ya tatu ilifanyika February 20.

Related Articles

Back to top button