BurudaniVideos

VIDEO: Simba SC wachukua mamilioni ya SportPesa, Ahmed Ally amtambia Tarimba

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam Sports Federation, Mapinduzi Cup na Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati Simba SC hii leo imepokea hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 50 kutoka kwa Wadhamini wao wa kuu SportPesa baada ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Mashindano ya CAF ikiwa kama bonasi kutokana na hatua waliyofikia.

Hii ni mara ya nne kwa Simba SC kuondoka na bonasi ya mzamini wao Mkuu SportPesa tangu walipoingia kandarasi ya miaka mitano.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas amewapongeza wachezaji na uongozi wa Simba SC kwa hatua waliyofikia.

Wakati CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez amewashukuru mabosi wao kwa zawadi hiyo huku akiamini kuwa wataweza kushinda Ubingwa wa Ligi Kuu na kuweza kuondoka na milioni 100 kama bonasi ambazo kwa miaka minne mfululizo wamekuwa wao ndiyo wakizipata mbele ya watani zao Yanga SC kutokana na kushinda kwao taji hilo la NBC.

Ahmed Ally kwa upande wake amemuhakikishia Tarimba Abbas kuwa watakapoingia kandarasi mpya basi watafanya kama walivyofanya safari hii kwa maana ya kuzichukua bonasi zote.

Kuangalia Full Video Ingia YouTube andika Bongo5

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button