Staa wa Klabu ya Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi amewataka vijana wa kitanzania wanaosakata kabumbu kutokata tamaa na wapiganie ndoto zao za soka bila maneno ya watu ambao wanawavunja moyo.
Hakimi yupo nchini na timu yake ya taifa ya Morocco kwaajili ya kuwakabili Tanzania hapo kesho majira ya saa 4 usiku katika kutafuta tiketi kuwania kufuzu Kombe la Dunia.