Events

Video: Uwezo wa askari wenye farasi wanogesha ‘Jiongeze Tukuongezee’, DStv wafanya kitu ‘Bab’kubwa

Wateja wa DStv wanaendelea kufurahia ofa kabambe zinazotolewa na MultiChoice na sasa imezindua kampeni mpya ya ‘Jiongeze Tukuongezee’ ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huunganishwa na kifurushi cha juu zaidi bila malipo ya ziada.

Kwa kampeni hii mpya iliyoanza rasmi tarehe 1 Machi 2020 na ambayo itaendelea hadi mwisho wa mwezi Aprili 2020, mteja wa kifurushi cha DStv Bomba Tsh 19,000 akilipia cha juu yake ambacho ni Family Tsh 29, 000 moja kwa moja ataunganishwa na kifurushi cha Compact Tsh 44, 000 bila malipo ya ziada.

Hivyo hivyo mteja wa kifurushi cha DStv Family, akilipia Compact atapandishwa kwenda Compact Plus Tsh 8400 na wakati yule wa Compact akilipia Compact Plus ataunganishwa kifurushi cha juu kabisa cha Premium cha Tsh 129, 000

”Kampeni hii ya Jiongeze Tukuongezee inakwenda sambamba na mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa wateja wetu kote nchini wanapata maudhui bora na mengi kadiri iwezekanavyo, kwa gharama nafuu kabisa,” amesema Hilda Nakajumo hii leo, wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo uliyofanyika katika ofisi za MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam.

Hilda amesema wanatambua kuwa kwa sasa wateja wana uzoefu na ufahamu wa maudhui bora na hali ya juu yanayo patikana kwenye vifurushi vya juu vya DStv, hivyo wameona ni vyema kuwapa wateja fursa ya kufurahia maudhui hayo kwa gharama nafuu.

Wateja wote wa vifurushi vya DStv Bomba, Family na Compact watanufaika na kampeni hiyo pale tu watakapo lipia kifurushi cha juu, hapo DStv itawapandisha kifurushi cha juu zaidi bila malipo ya ziada. Wateja wa kifurushi cha Compact Plus wataendelea kunufaika na Chaneli za kifurushi cha juu cha Premium wakati wote wa kampeni hii.

Kwa Ofa hii, mwezi Machi utakuwa mwezi maalum kwa kila mteja wa DStv. Kila mtu atakaye jiongeza na kulipa kifurushi cha juu atapandishwa ngazi na hivyo kupata maudhui ya kifurushi cha juu zaidi. Hii itawafanya wateja wa DStv kushuhudia maudhui kabambe kama vile Ligi kubwa za kandanda duniani, michezo kama ndondi, mieleka, tenis, riadha bila kusahau sinema na tamthilia mbalimbali maarufu duniani pamoja na chaneli za Habari, Utafiti na Elimu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents