Habari

Video: Watu waliichukulia hiii serikali poa, sasa serikali yetu itaendeshwa kwa matendo makali – Rais Samia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mawaziri wateule wanne na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Mawaziri ni Dkt. Stergomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, January Makamba Waziri wa Nishati, Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi na Dkt. Ashatu Kijaji Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pia, Dkt. Eliezer Feleshi amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametaka kuwepo Mikataba bora ya Nishati hususan ya Umeme. Amesema hayo wakati wa Uapisho wa Viongozi walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema, “Tuna matatizo makubwa kwenye Nishati ya Petroli, Dizeli na jamii zake zote. Bei ya Petroli isipande kama inavyokwenda, tuangalie mbinu mbadala”

 

“Serikali yetu itaendeshwa kwa matendo makali na siyo maneno makali, ninaposema matendo makali wala siyo kupigana mikwaju au mijeledi ni kwenda kwa wananchi na kutoa huduma inayotakiwa kila mtu afanye wajibu wake”, Rais Samia

“Katika kipindi cha miezi sita kuna watu waliichukulia hiii serikali poa, serikali cool, watu wakafanya wanayoyataka… kutokana na jinsi nilivyoona utendaji wa mawaziri na viongozi wengine kwenye wizara, [mabadiliko haya] bado yatakuwa yanaendelea.”- Rais Samia Suluhu Hassan

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents