Video: Wizkid asema yuko tayari kufanya collabo na Davido

Licha ya Wizkid na Davido kuwa wapinzani wakubwa kimuziki nchini Nigeria, lakini kuna uwezekano mkubwa wa siku moja kusikia wamefanya collabo.

Wizkid amesema upo uwezekano wa yeye kufanya ngoma na Davido, baada ya kuulizwa kama inaweza kutokea siku moja yeye na Davido wakatakiwa kufanya ngoma ya pamoja.

Wizkid aliulizwa na Dj Abrantee kwenye mahojiano na Capital Xtra ya UK, “Kama ikitokea nafasi ya nyinyi wawili kufanya wimbo wa pamoja, itawezekana?” na jibu lake lilikuwa “Kila kitu kinawezekana duniani, tutaona.”

Related Articles

Back to top button