Habari

Vifaa tiba vya Tsh Mil. 180 kutolewa siku ya Mtoto Njiti

Doris Mollel Foundation leo, wamezindua maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo kwa kawaida huadhimishwa mnamo tarehe 17 Novemba kila mwaka.

Kwao, maadhimisho hayo yatafikia kilele mnamo tarehe 20 Novemba 2022 na yatafanyika katika viwanja vya Robanda, vilivyopo katika Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara.

Katika siku hiyo, Doris Mollel Foundation, wamejipanga na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zitaambatana na kukabidhi misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo nchini, ambao ni; TIKA, Aga Khan Hospital, Oryx Energies Tanzania, Freo2 Foundation, Miracle Experience, Coca Cola Tanzania, Precision Air Tanzania, Anudha Limited, Ashton Media, Nest360, na Ifakara Health Institute, ambao kimsingi, wanawashukuru sana kwa kuwaunga mkono katika kuhakikisha kuhakikisha maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti yanafana.
Katika maadhimisho hayo, Doris Mollel Foundation itakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 180,190,000 ambavyo vitakwenda katika hospitali za Wilaya za Serengeti, Ukerewe, Kwimba, na Magu, pamoja na ufungaji wa mitambo ya hewa oxygen kwa watoto wachanga katika hospitali za Siha, Karatu, Monduli na Dabaldi; pia itakabidhi mitungi 200 ya gesi yenye thamani ya shilingi 8,200,000 kwa ajili ya akina mama wajawazito katika Wilaya ya Serengeti; itaungana na wadau wa maendeleo katika kupanda hot air balloon na kutalii hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kukuza utalii na kuhamasisha kujitolea, na kupandisha ujumbe wa watoto njiti katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
Kwa ujumla maadhimisho haya yamegharimu shilingi 236,230,000 ambapo shilingi 180,190,000 ni vifaa tiba, shilingi 8,200,000 ya mitungi ya gesi, na shilingi 47,840,000 ni gharama za shughuli nzima, usafiri, matangazo ya mtanda, kupanda hot air balloon, malazi, na chakula.
Bi. Doris Mollel, ambaye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, amewashukuru sana wadau wote wa maendeleo kwa moyo wao wa kujitoa na kuwasihi waendelee na moyo huo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents