Vifahamu visiwa vinavyosifika kwa kutembelewa na wapendanao (+ Video)

Filicudi na Stromboli ni visiwa vyenye mandhari ya kuvutia, vikipatikana katika bahari ya Pacific katika taifa la Italia.

Visiwa hivi viwili vimeundwa na vilima vya volcano na wakati mwingine hupata milipuko midogo lakini milipuko haitokei kwenye vilima vyote.

Harugu ya mimea Cestrum nocturnum yenye manukato ya kuvutia iliyotanda kwenye visiwa hivi inasemekana kuwasaidia watu kupumzika, kukabiliana na msongo wa mawazo na kupunguza hali ya mchoko na wasi wasi wanaokuwa nao katika pilikapilika za maisha ya kila siku.

Unapotembelea visiwa hivi harufu ya mimea ya maua ya jasmini inayotoa harufu ya kuvutia husasan nyakati za usiku

Wenyeji wa visiwa hivi vinavyopatikana katika katika Sicily, wamekuwa wakiwaelezea waandishi wa habari kuwa sio visiwa vya kawaida, kwani huchochea msisimuka wa mapenzi hususan kwa wapendanao wanapovitembele kujivinjari kwa mapumziko.

Wanasema wanajivunia kuwa katika visiwa hivyo wanavyoviita “mtoto wa volkano,” na wanajivunia nguvu za mmea, ambao wanasema unaongeza nguvu za kiume. Mara nyingi hupenda kutoa mzaha kwamba kisiwa chao “kila wakati kina joto.”

Unapotembelea visiwa vya Stromboli and Filicudi tarajia kuendeshwa kwenye mawimbi masafi yanayong’ara ya rangi ya blu yenye mvuto.

Wavuvi wenyeji wa visiwa hivi wanafahamika kwa kuwatembeza wenzi wanaovitembelea hadi kwenye “mapango ya uzazi.”

Na kama wewe ni mwanamke au msichana ambaye hujapata mchumba, wavuvi katika visiwa hivi basi watakutembeza kwenye boti hadi kwenye miamba yenye maumbile yasiyo ya kawaida ambayo inasemekana unapoyagusa hukupatia bahati katika kutafuta mpenzi.

Ni eneo lenye asili isiyo ya kawaida. Kuna kijiji kimoja tu uvuvi, Pecorini a Mare, chenye nyumba ziliopakwa rangi, bandari mbili ndogo na barabara moja pekee inayozunguka kisiwa.

Visiwa hivi pia huwavutia mashabiki wa kupanda miamba na ni makao ya mijusi nyoka wa kipekee ambao huwavutia sana wageni wanaovitembelea.

Hizi ni baadhi ya picha za kuvutia za visiwa vya visiwa vya ”hija ya wapenzi” vya Italia.

Bofya hapa chini Kutazama.

https://www.instagram.com/p/CTZq2u6jMeb/

Related Articles

Back to top button