Habari

Vikwazo kutoka nchi za Magharibi havituathiri kitu – Urusi 

Urusi imesema vikwazo vya nchi za magharibi havina athari kwake na imeapa kujibu kwa namna yake kufuatia ripoti kwamba Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zinatayarisha vikwazo vipya dhidi yake.

Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov amesema wale wanaotegemea vikwazo wanapaswa kutafakari tena na wajiulize je, wanatimiza lengo lolote kwa kuendelea na sera kama hiyo ?

Ameongeza kuwa bila shaka sera kama hiyo haifanikishi malengo yake. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov naye amesema bila shaka Urusi itajibu hatua yoyote kutoka nchi za Magharibi.

Wiki hii nchi za Umoja wa Ulaya ziliidhinisha vikwazo kutolewa dhidi ya maafisa wanne wa ngazi za juu wa Urusi kwa kuhusika na hatua ya kumuweka kizuizini mkosoaji mkuu wa serikali ya Putin Alexei Navalny.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents