HabariSiasa

Viongozi wa Afrika Mashariki kujadili mzozo wa DR Congo

Viongozi wa mataifa saba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki watakutana leo Jumatatu mjini Nairobi kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkutano huo unakuja wakati kumezuka mapigano makali yanayofufua uhasama wa miongo kadhaa kati ya Kinshasa na Kigali, huku DRC ikiilaumu Rwanda kutokana na kuibuka upya hivi karibuni kwa kundi la waasi la M23.

Rwanda imekanusha mara kwa mara kuwaunga mkono waasi hao huku nchi zote mbili zikilaumiana kwa kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka.

Ofisi ya rais wa Kenya imesema watu wa mashariki mwa DRC wameteseka kwa muda mrefu na wanaendelea kulipa gharama kubwa kupita kiasi kwa kupoteza maisha, mali na amani.

Siku ya Jumatano, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa wito wa kutumwa mashariki mwa DRC kikosi cha kikanda ili kurejesha amani, lakini Kinshasa ilisema haitakubali kamwe ushiriki wa Rwanda katika operesheni hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents