HabariSiasa

Viongozi wa Afrika Mashariki wakubaliana kupeleka jeshi DRC

Wakuu wa mataifa ya Afrika Mashariki wamekubaliana jana Jumatatu kupeleka jeshi la kikanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kujaribu kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo.

Wakuu wa mataifa ya Afrika Mashariki pamoja na kukubaliana kuanzisha jeshi hilo, wametoa pia mwito wa kusimamishwa mapigano mara moja. Wakuu hao walikutana jijini Nairobi kujadili hali ya usalama kwenye eneo hilo.

Hatua hiyo imetangazwa na ofisi ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya wakuu wa mataifa saba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya mazungumzo kuhusiana na kuongezeka kwa machafuko katika eneo hilo tete. ambayo pia yanatishia hali kwenye mataifa jirani.

Sehemu ya taarifa hiyo imesema wakuu hao wameliagiza jeshi hilo la kikanda kwa kushirikiana na vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kurejesha utulivu na kuhakikisha amani nchini humo. Wakuu hao aidha, wameagiza kusimamishwa mapigano lakini pia kuondolewa kwa uhasama mara moja.

Rwanda inahusishwa?

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema chochote kuhusiana na iwapo wanajeshi kutoka Rwanda watahusishwa kwenye jeshi hilo la kikanda, ingawa tayari serikali ya Kongo inasisitiza kwamba hawataki kuona wanajeshi hao wakijumuishwa.

Sehemu ya taarifa ya ofisi ya rais wa DRC, Felix Tshisekedi imesema jeshi hilo linatakiwa kuanza operesheni zake katika kipindi cha wiki zijazo, na lisijumuishe chochote kutoka jeshi la Rwanda.

Marais wa Rwanda Paul Kagame na Felix Tshisekedi walihudhuria mazungumzo hayo ya Nairobi yaliyoandaliwa na rais Kenyatta. Pamoja nao ni wakuu wa mataifa ya Burundi, Sudan Kusini na Uganda, pamoja na Tanzania iliyowakilishwa na balozi wake nchini Kenya.

Kagame alihudhuria, licha ya Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano unaowakutanisha wakuu wa serikali za Jumuiya Madola kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni, CHOGM, baadae wiki hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents