HabariSiasa

Viongozi wa upinzani Madagascar mbaroni kwa maandamano

Polisi ya Madagascar jana iliwakamata kwa muda wanasiasa wawili vigogo wa chama kikuu cha upinzani wakati wa maandamano ya umma yaliyofanyika kwenye mji mkuu kulalamika juu ya hali ngumu ya kiuchumi na kupanda kwa gharama ya maisha.

Polisi ilisema imewatia nguvuni Rina Randriamasinoro, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha upinzani cha TIM pamoja na mratibu wa chama hicho ngazi ya taifa kufuatia vurumai iliyozuka kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Mamia ya waandamanaji wanaoipinga serikali walikusanyika katikati mwa mji mkuu Antananarivo huku wakifuatiliwa kwa karibu na idadi kubwa ya maafisa wa jeshi na polisi.

Kukamatwa kwa viongozi hao kulichochea zaidi maandamano huku waandamanaji wakiahidi kutoondoka eneo hilo hadi viongozi hao wawili watakapoachiwa.

Hata hivyo iliarifiwa kuwa waandamanaji walitawanyika majira ya mchana na viongozi hao wa upinzani waliachiwa huru baadaye jioni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents