Habari

Viongozi Wakuu Chadema waiomba Mahakama Kuu ifanye marejeo ya mwenendo wa kesi (+video)

Maombi ya marejeo namba 126/2018 yaliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam na Viongozi Wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa CHADEMA, leo Ijumaa, Julai 6, 2018 yamefikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa ambapo shauri limeahirishwa hadi Julai 13, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.


Wakati huo huo upande wa wafungua maombi wakiwakilishwa na Mawakili Peter Kibatala na Jeremia Mtobesya, Freddy Kihwelo na Hekima Mwasipu, umeomba kuongeza masuala mengine kwenye kiapo chao (supplementary affidavity) ifikapo leo jioni, kisha upande wa wajibu maombi (Jamhuri) utawasilisha kiapo kinzani siku ya Jumatatu, Julai 9, mwaka huu.

Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam pia imetoa muda wa kuanzia Jumatatu Julai 9 na hadi Julai 11, kwa upande wa wafungua maombi kufanya ‘reply’ baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha kiapo kinzani, kabla ya shauri hilo kuanza kusikilizwa Ijumaa, Julai 13 mwaka huu.

Wafungua maombi wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe wamefungua shauri hilo kuiomba Mahakama Kuu ifanye marejeo ya mwenendo wa kesi na. 112/2018 inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Wengine katika shauri hilo la maombi ya marejeo na. 126/2018 ni; Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji, NKMB John Mnyika (Mb) NKMZ Salum Mwalim, Mkiti wa BAWACHA Halima Mdee (Mb), Peter Msigwa (Mb), Esther Matiko (Mb), John Heche (Mb), Esther Bulaya (Mb).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents