Habari

Virusi vya Corona vyaathiri soko la mafuta, Urusi na Saudi Arabia kupunguza uzalishaji

Shirika la nchi zinazozalisha na kuuza mafuta kwa wingi duniani – OPEC na Urusi wanakutana leo kujaribu kukubaliana kuhusu kupunguzwa kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa mafuta lakini juhudi zao za kushughulikia kuanguka kwa bei za bidhaa hiyo kutokana na janga la virusi vya corona zimevurugwa na uhasama wa pande zote na kusita kwa Marekani kujiunga na hatua hiyo.

Mahitaji ya mafuta duniani kote yamepungua kwa asilimia 30 huku hatua za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona zikisitisha safari za ndege, kupungua kwa matumizi ya magari na kupunguzwa kwa shughuli za kiuchumi.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha DW, Bei za mafuta ghafi zimeshuka chini ya gharama za uzalishaji kwa mataifa mengi, ikiwemo sekta inayonawiri ya mafuta nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema wiki iliyopita kuwa amefikia makubaliano kati ya Urusi na Saudi Arabia kupunguza kwa mapipa milioni 10 hadi 15 ya mafuta ghafi kwa siku, au asilimia 10 hadi 15 ya mafuta yanayouzwa duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents